Mazishi ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela yalitumiwa kama mwanya wa ‘wapiga dili’ kujipatia mamilioni kwa ufisadi, ripoti imebaini.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa wiki iliyopita na ‘Public Protector’ inayoongozwa na Busisiwe Mkhwebane, zaidi ya Rand Milioni 3 (R3000 Million) zilipotea au kutumiwa kwa matumizi yasiyo halali kwa mgongo wa msiba huo ulioigusa dunia.

Imeelezwa kuwa kulikuwa na matumizi mengi hewa huku fedha zikitolewa kulipia bidhaa hewa.

Ripoti ya Mkhwebane iliitaja kampuni ya Reagola Print And Mail, ambayo ilidai kuwa ilitoa huduma ya fulana na baadae kupunguza idadi, iliwasilisha hati ya malipo ya mamilioni ya fedha (R 1.9 Million) ambayo siyo madai halali.

 

Imeeleza kuwa kwenye vitabu vya mahesabu vya serikali, mazishi hayo yamewekwa kama tukio la dharura, hivyo kutoa mianya mingi iliyotumiwa na ‘wapiga dili’ kufuja fedha.

Mzee Mandela alifariki Disemba 5 mwaka 2013 na alizikwa Disemba 15 mwaka huo.

AAR na Jema Foundation watoa msaada kwa watoto wenye Saratani
Video: Mbunge amwaga mboga CUF, ataja sababu za kujiuzulu