Vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimemvua taji la miba waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyetangazwa kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kupitia wenyeviti wa vyama vinavyounda umoja huo ambao waliwahi kumtuhumu Lowassa kuwa ni fisadi aliyehujumu uchumi wa Tanzania kwa miaka mingi, jana wenyeviti hao wamemkaribisha kwenye ngome yao yakimsafisha kama mwanakondoo aliyekuwa anaonewa katika zizi alilokuwepo.

Akisoma tamko la kumkaribisha rasmi kwenye ngome hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa alisema wako tayari kushirikiana nae katika umoja huo.

“Tunamchukua fursa hii ya kipekee kumwalika Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Lowassa ajiunge na Ukawa na ktuko tayari kushirikiana naye katika kuhakikisha kuwa tunaiomdoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao,” alisema Mbatia.

“Ni rai ya Ukawa kwa kila Mtanzania ambaye yupo tayari kuuondoa mfumo huo kandamizi na dhalimu wa CCM kushirikiana na Ukawa kwa lengo la kujenga Taifa imara. Ukawa ndilo tumaini la Watanzania, tusikubali kunyamaza pale sauti zetu zinaponyamazishwa kwa lazima na bila sababu, tusikubali kunyimwa fursa ambazo tuna uwezo nazo, tuwe tayari kushiriki michakato ya kimekrasia ya kuleta mabadiliko na kupata viongozi bora,” aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi – CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alimsafisha Lowassa kwa kueleza kuwa yeye sio chanzo cha tatizo la ufisadi bali ni tatizo ni mfumo wa CCM huku akimtaja kama mchapakazi ambaye kazi yake inajulikana kwa umma wa watanzania.

Kutokea (Kushoto) Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi, Mh Profesa Ibrahim Lipumba, Mh. Freeman Mbowe, Mhandisi James Mbatia, Mh. Jhn Makaidi, Mh. Juma Duni Haji na Mh. Said Issa Mohamed wakionesha mshikamano wakati wa mkutano wa kumkaribisha Mh. Edward Lowassa uliofanyika mako makuu ya CUF Buguruni Dar es Salaam leo.

Kutokea (Kushoto) Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi, Mh Profesa Ibrahim Lipumba, Mh. Freeman Mbowe, Mhandisi James Mbatia, Mh. Jhn Makaidi, Mh. Juma Duni Haji na Mh. Said Issa Mohamed wakionesha mshikamano wakati wa mkutano wa kumkaribisha Mh. Edward Lowassa uliofanyika mako makuu ya CUF Buguruni Dar es Salaam leo.

“Lowassa alijiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008, tujiulize tangu amejiuzulu, je, ufisadi umeongezeka au umepungua ndani ya serikali ya CCM? Hili ni suala la kimfumo tu ambalo linasababisha ufisadi ndani ya CCM,” alisema Prof. Lipumba.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye alikaririwa akimtuhumu Lowassa kuwa ni fisadi katika majukwaa mbalimbali ya kisiasa, alikataa kuzungumza chochote kwa madai kuwa wenyekiti wenzake wameshazungumza yote kwa kina.
Lowassa ambaye anatarajiwa kuwa mgombea urais wa Ukawa baada ya kujiunga na Chadema, amepanga kuzungumza leo kwenye mkutano maalum ambao unatarajiwa kurushwa na kituo kikubwa cha runinga kinachoonekana katika mikoa yote ya Tanzania.
Ukawa wanatarajia kumtangaza rasmi mgombea wao Agosti 8 mwaka huu.

Simba Yajipeleka Kimataifa Kidijitali
Mkongo Mangulu Atua Newcastle United