Majibu ya utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya ‘East African Institute’ nchini Kenya imetoa matokeo ambayo yamewashitua wengi kuhusu muelekeo wa nchi hiyo katika vita dhidi ya rushwa.

Kwa mujibu wa utafiti huo,ikiwa umebaki mwaka mmoja tu nchi hiyo ifanye uchaguzi mkuu, asilimia 40 ya vijana wa Kenya wamekiri kuwa watampigia kura mgombea ambaye atawapa rushwa.

Utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 50 ya vijana wa Kenya pia wanaamini kuwa haijalishi ni njia gani mtu anatumia kutengeneza pesa ili mradi anaweza kukwepa kwenda jela huku asilimia 47 wamesema kuwa wanawakubali sana au wanawapenda watu wanaotengeneza pesa kwa njia haramu.

Kingine kilichowashitua wakenya ambao hivi karibuni rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta alitangaza rushwa kuwa adui wa taifa, asilimia 30 ya watu waliohojiwa walidai kuwa rushwa ina faida wakati asilimia 35 walidai wako tayari kupokea na kutoa rushwa.

“Hiki ni kizazi ambacho hakioni tabu kuhusu kukwepa kodi na kutoa au kupokea rushwa,” alisema Dk. Awiti ambaye ni Mkurugenzi wa East African Institute.

 

 

Inter Milan Watangaza Kuachana Na Nemanja Vidic
Picha: Mchungaji amchoma moto muumini akidai amesikia sauti ya Mungu