Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameamua kumjibu mgombea urais wa Marekani, Donald Trump ambaye hivi karibuni alidai kuwa akiingia madarakani atahakikisha anawakamata na kuwafunga yeye na rais mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni.

Mugabe alitumia hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo iliyofanyika jijini Harare juzi (Januari 3) kumjibu Trump. Alisema kuwa Trump ana damu ya Hitler.

Hivi ndivyo alivyoeleza:

“Hivi karibuni yule mwendawazimu anayetaka kuwa rais wa Marekani alisema kuwa atawakamata baadhi ya marais wa Afrika akiwemo kaka yangu Yoweri na mimi na kutufunga gerezani endapo atakuwa rais.

“Naomba nimueleze hapa kwamba Trump hataweza kutupeleka popote kwa sababu sisi waafrika ni imara zaidi duniani na hatuogopi. Ningependa kila mmoja kufahamu kuwa sina cha kuogopa na nataka niiambie dunia kuwa huyo mzimu wa Hitler umemchukua na anakaribia kufanya ya hovyo watu wa Marekani wakimchagua.

“Kama ambavyo babu yake Hitler alivyosababisha vita ya pili ya dunia, na yeye anataka kuanzisha vita ya tatu ya dunia ili aache kumbukumbu lakini dunia haitaruhusu hilo.

“Hivi inakuaje unaanza hata kufikiria kuwa utamkamata mtu kama mimi? Hivi kichwa cha Trump kiko sawa? Na… hivi kuna madaktari wa kutosha Marekani kumpima ukichaa huyu mtu?

Madaktari Wagundua tiba ya Ukimwi, Wagonjwa wawili wapona
Samia Suhulu Atua Mgodini, Awaacha na 'neno'