Mashetani wekundu Man Utd, huenda wakahamisha silaha zao za usajili huko nchini Ureno, na kuachana na mshambuliaji kutoka nchini Hispania pamoja na klabu ya Barcelona, Pedro Rodrigues.

Manchester United, wametajwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa na mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Argentina pamoja na klabu ya Benfica ya nchini Ureno, Osvaldo Nicolás Fabián “Nico” Gaitán kwa ada ya usajili wa paund million 28.

Gazeti ya nchini Ureno liitwalo A Bola, limevunjisha siri hizo ambazo zilidakwa na waandishi wa habari wa gazeti la The Sun la nchini England ambalo limesisitiza juu ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Taarifa hizo zinadai kwamba, Gaitan ameshaanza kuwaaga baadhi ya wachezaji wenzake wa Banfica kwa kusisitiza yu njiani kuondoka na kwenda kujiunga na klabu iliyo nje na nchi ya Ureno.

Gaitan, anakususdiwa kushika pahala pa mshambuliaji aliyeondoka Old Trafford juma lililopita, Angel di Maria ambaye alijiunga na mabingwa wa soka nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain kwa ada ya usajili wa paund million 46.

Gazeti hilo limeongeza kwamba, mipango ya usajili wa Gaitan imeongezewa chachu na falsafa za meneja wa Man Utd, Louis Van Gaal ya kupendezwa na hatua ya kufanya kazi na wachezaji kutoka nchini Argentina.

Mpaka sasa meneja huyo ameshawasajili wachezaji kadhaa kutoka nchini Argentina tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Man Utd, mwezi June mwaka 2014.

Euro 2016 Kumfukuzisha Hodgson
Kikwete Na Lowassa, Mkono Kwa Mkono...?