Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athuman Kihamia amesema kuwa tume hiyo imejipanga vizuri katika uchaguzi wa marudio katika jimbo la Liwale na baadhi ya Kata .

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri.

Amesema kuwa kwasasa tume inafanya kazi ya kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu haki yao ya msingi ya kupiga kura.

“Maandalizi yameenda vizuri, kilichobaki sasa hivi tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ni kutoa elimu tu ya mpiga kura,”amesema Kihamia

Mafuriko ya matope yaua 8
Huddah amtaka Kenyetta ahalalishe bangi