Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kumuua jambazi aliyeongoza mauaji ya Polisi 8 yaliyotokea Wilayani Kibiti mkoani Pwani baada ya kumsaka kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa hii leo na Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema baada ya kumsaka kwa muda mrefu jambazi huyo sugu ajulikanaye kwa jina la Rashid Kapela hatimaye jeshi hilo lilifanikiwa kumuua katika maeneo ya Kivule Chanika jijini humo.

“Baada ya kupewa taarifa na wasamalia wema, Jeshi hilo lilifika na kuizingira nyumba alimokuwa lakini alifanikiwa kutoka na kutaka kutoroka akitoro Polisi walipomsimamisha alikimbia ndipo wakampiga risasi ya goti na kuanguka, alipohojiwa aliwataja wenzake pamoja na matukio makubwa ya uhalifu aliyoshiriki kuyafanya likiwemo hilo la mauaji ya askari Polisi wanane na kupora silaha zao kisha kukimbia,” amesema Kamanda Mambosasa.

Video: Mlinzi wa Meja Jenerali Mstaafu Vicent ashikiliwa na Polisi
Mugabe amzuia msanii wa kike kuingia Zimbabwe kwa kutovaa nguo za ndani