Kampuni ya simu ya Tecno imewafahamisha wateja wake kufika katika tamasha la Simu Expo linalofanyika leo Viwanja Posta ( Kijitonyama) ili wakapate kufahamu kuhusu simu halisi na simu bandia ambazo hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itazifungia.

Kampuni hiyo imewatoa wasiwasi wateja wake kuwa simu zao ni halisi na kinachotakiwa ni wewe kusogea maeneo ya viwanja vya Posta ( Kijitonyama) ili ukapate kufahamu jinsi ya kuzitambua simu halisi na bandia, pia wameipongeza TCRA kwa hatua ya kuzifungia simu bandia kwani itawasaidia watanzania kupata bidhaa halisi kwa matumizi

Uhaba wa sukari kumalizika nchini
Kangi Loguola alia na Kodi kwa Wabunge, adai watarudi kuwa ombaomba