Msanii toka kundi la WCB, Rajabu maarufu kama Harmonize amekuja na ngoma mpya aliyomshirikisha msanii toka Nigeria anayeitwa Korede Bello anayefanya vizuri barani Afrika.

Koredo Bello alitambulika zaidi baada ya kufanya ngoma iliyojulikana kwa jina la Godwin, pia amewahi kufanya  kibao cha Romantic alichomshirikisha mwanadada Tiwa Savage, hivi karibuni aliaachia wimbo wake unaoitwa do like that.

Tangu kuachiwa kwa ngoma ya shulala, katika mtandao wa YouTube ndio ngoma inayofanya vizuri na kushika namba moja kwa upande wa Tanzania huku ikiwa imekwisha tizamwa na watu 223,528.

Harmonize sasa anafanya vizuri kwa kufuata nyayo za Boss wake Diamond Platinumz ambae hivi karibuni anatarajia kuachia ngoma yake mpya akiwa na Rick Ross.

Tazama ngoma hiyo, Harmonize Ft Koredo Bello, wimbo unaitwa Shulala.

Nyumba za ibada zakumbwa na bomoabomoa leo
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 16, 2017