Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imewaagiza wafanyabiashara wote wanaojihusisha na uuzaji wa silaha za jadi barabarani kuacha tabia hiyo mara moja na badala yake kutafuta sehemu maalumu ya kufanya biashara hizo,tabia hiyo imejengeka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujihusisha na uuzaji wa siraha kama mapanga, visu, manati na upinde pembezoni mwa barabara hususani kwenye mataa ya kuongozea magari.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Saimon Sirro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, amesema kuwa biashara hizo zimekuwa hatarishi kwa usalama wa watu wanaotumia Barabara hizo, pia ameongeza kuwa biashara hizo  zimeshamiri sana katika makutano mbalimbali ya Barabara jijini Dar es salaam.

“Nimepiga marufuku uuzwaji wa bidhaa hizo kwasababu watu wanao husika na uuzaji wa bidhaa hizo wamekuwa sio waaminifu na hutumia fursa hiyo kuwatishia watu wanaokuwa kwenye magari binafsi na magari ya umma na kuanza kuwaibia mali zao mbalimbali kama simu za mikononi, Saa, Mikoba na Laptop,”amesema Sirro.

Vile vile Sirro amesema ameongeza kuwa kikosi cha usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam ya ukamataji wa makosa barabarani katika kipindi cha January 5 hadi January 12 wamefanikiwa kupata Fedha  za tozo sh. Milioni 657,060,000
Hata hivyo Kamishna Sirro amesema silaha hizo zinatakiwa kuuzwa kwenye maduka yenye leseni na sio vinginevyo ambapo atakayepatikana akifanya biashara hiyo atachukuliwa hatua za kisheria

Wizara yamkingia kifua Prof. Muhongo
Video: NEC yatoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya ACT-Wazalendo