Waislamu duniani kote kuadhimisha siku ya ‘QUDS’ leo mosi ikiwa ni maadhimisho ambayo huwa yanafanyika kila mwaka, lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kupinga kile kinachoendelea huko palestina.

Hayo yamesema na Sheikh Hemed Jalala alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  na kutoa wito kwa waislam wote kufanya maandamano ya amani siku ya ijumaa(leo) ya mwisho wa mwezi wa ramadhani kwaajiri ya kupinga kile kinachoendelea huko palestina na kuombea amani nchi hiyo.    

“Tukio la QUDS ni jambo la uwanaadam, halimhusu tu Muislamu, halimhusu tu Mkristo, bali linamhusu hata asiye kuwa na dini. Matatizo wanayokumbana nayo waislamu wa Palestina na Wakristo wanaoishi Palestina kwakweli ni matatizo ambayo sisi kuyanyamazia ni kunyamazia haki” – Sheikh Hemed Jalala

Video: Mahakama ya Mafisadi rasmi leo. Wabunge watatu wa CHADEMA wafungiwa - Magazeti leo
Serikali yaagiza Halmashauri kukusanya mapato 'kielektroniki'