Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amewataka wakulima wa zao la zabibu na wachakataji kufanya ukulima wenye tija kwa kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani kwani zao hilo limeongezeka thamani baada ya serikali za kuwatafutia masoko ya uhakika wazalishaji na wakulima.

Mavunde ameyasema hayo katika mazungumzo hayo na kuwataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanashirikiana vizuri, ili kuweza kuleta maendeleo ya ndani ya Mkoa na Taifa kitu ambacho kitasaidia pia kukuza patola mtu mmoja mmoja.

Amesema, ’’Serikali hatuwezi kuweka siasa kwenye Maisha ya watu lazima mikakati yetu ijibu changamoto zinazowakabili wakulima ili mwisho wa siku waweze kwenda mbele kwa kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi.’’

Zabibu hulimwa kwa wingi Mkoani Dodoma na ndio mkoa pekee unaolima Zabibu kwa wingi nchini na hata kwa afrika mashariki ukiwa mkoa wenye utajiri mkubwa wa zao hili kitu ambacho ni fursa kwa wananchi wa Mkoa huo kulitilia mkazo ulimaji wa zao hili ili liweze kuinua uchumi wa wananchi, mkoa na Taifa kwa ujumla.

Simba SC yatakaa kumtoa Joash Onyango
5,000 yampa Tsh 20,000,000 kwa kucheza Kasino ya Meridianbet