Wanawake nchini Marekani wamepewa fursa ya kujiunga na jeshi la nchi hiyo na kuingia vitani kupambana mstari wa mbele.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ash Carter huduma za kijeshi za Marekani hazitaweza tena kupunguza nusu ya watu wenye ujuzi na vipaji.

Kwa mujibu wa BBC, Carter amesema kuwa wanawake sasa wanaweza kuendesha magari ya kijeshi vitani, mizinga na kuongoza askari wa nchi kavu kwenye mapambano.

Mpango huo wa kuwaweka wanajeshi wanawake msitari wa mbele, unatofautiana na hoja ya mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Majeshi kuwa kikosi cha maji kinaweza kuwatenga wanawake katika baadhi ya majukumu.

TRA Yasitisha Safari Ya Timu Ya Taifa Ya Vijana
Watuhumiwa Upotevu wa Makontena 349 Wapandishwa Kizimbani