Wapenzi  wa jinsia moja nchini Afrika Kusini wamekuwa wa kwanza duniani kujifungua watoto watatu kutoka kwa vinasaba vya DNA vya wanaume hao wawili ,kulingana na taarifa iliyotolewa na jarida la Gay Times.

 Mwezi Julai mama aliyebeba mimba ya watoto hao ambao wawili ni mapacha alijifungua na kuwashangaza watu wengi ambapo  kitendo hicho kilionekana kuwa siyo cha kawaida.

Jarida hilo lilisema kuwa  wapenzi hao wa jinsia moja walikutana na mama aliyebeba mimba hiyo kupitia kwa mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ambaye ni jirani yao.

Christo na Theo Menelaou walikutana na mama aliyebeba mimba hiyo katika sherehe ya  ndugu na marafiki wa Oscar Pistorius baada ya kesi ya mwanariadha huyo kumalizika

Mbwa Achaguliwa Tena Kuwa Meya Minnesota, Marekani
Jaji Mutungi Kutafuta Suluhu Ya Maandamano,Aahidi Kufanya Vikao Mfululizo