Orodha kamili ya timu zitakazoshiriki fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (2019 Under-17 Africa Cup of Nations finals), imefahamika rasmi, baada ya kukamilika kwa michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali hizo ukanda wa Afrika ya Magharibi (Kanda A).

Wenyeji wa michezo ya kuwania kufuzu ukanda wa Afrika magharibi (Kanda A) Senegal wamefanikiwa kujihakikishia kucheza fainali za vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kuichabanga Guinea mabao manne kwa sifuri.

Hata hivyo nchi ya Guinea itashiriki fainali hizo kwa mujibu wa kanuni na sheria za michuano ya Afrika kwa vijana hatua ya kufuzu kupitia ukanda huko (Kanda A).

Senegal na Guinea wanajiunga na Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika Magharibi (Kanda B), baada ya vijana wa taifa hilo kuifunga Ghana katika mchezo wa hatua ya fainali mwishoni mwa juma lililopita.

Mataifa hayo ya Afrika magharibi yanaungana na mataifa mengine ambayo tayari yameshafuzu kucheza fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kupitia kanda nyingine za bara hilo, Tanzania (Mwenyeji), Uganda (Cecafa – Afrika mashariki), Senegal (Wafu Kanda A – Afrika Mafgharibi)   , Morocco (Unaf – Afrika Kaskazini), Guinea (Wafu – Kanda A – Afrika Magharibi), Angola (Cosafa – Afrika kusini), Nigeria (Wafu – Kanda B – West) na Cameroon (Uniffac – Afrika ya kati)

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linatarajia kupanga makundi ya fainali hizo baadae mwaka huu.

Fainali za Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa mwaka 2019 nzimepangwa kuanza kuunguruma Mei 12 jijini Dar es salaam, na timu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa umri huo, zitakazorindima nchini Peru.

Ndugulile: Majibu ya Malaria, U.T.I, Typhoid mengi siyo kweli
Kisa cha wazazi wa mwanafunzi darasa la tatu kutiwa mbaroni