Bi Aida Hadzialic, ambaye ni waziri wa elimu nchini Sweeden amejiuzulu baada ya kukamatwa na polisi Malmo akiwa anaendesha gari huku amelewa.

Taarifa hiyo ya kujiuzulu kwa waziri huyo imevuta hisia za watu wengi zaidi, Bi Hadzialic , ambaye ndiye waziri kijana zaidi kuteuliwa kushika nafasi hiyo nchini humo, amesema ni lazima awajibike  kwa alichokifanya kwani ni kosa kubwa zaidi alilowahi kulifanya maishani mwake.

Alipimwa na kugunduliwa kwamba alikuwa tu amepitisha kidogo kipimo kinachoruhusiwa cha unywaji pombe.

Sweden huwa na sheria kali sana za kuzuia uendeshaji gari mtu akiwa amelewa.

Bi Hadzialic, aliyehamia Sweden kama mkimbizi Mwislamu kutoka Bosnia Herzegovina akiwa mdogo, amesema alikuwa amekunywa gilasi mbili pekee za mvinyo

Mapigano Yamezuka Baina ya Pande Hasimu Nchini Sudan Kusini
Mo Farah Aweka Rekodi Kwa Kushinda Mbio Za Mita 10,000