Hali ya kisiasa Zanzibar inaendelea kutoa sura tofauti kadri siku zinavyozidi kwenda huku pande zinazovutana zikitoa taarifa tofauti kuhusu kinachoendelea katika mazungumzo ya kutafuta muafaka baada ya mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema kuwa tayari bajeti ya uchaguzi wa marudio visiwani humo imeshatengwa na kinachosubiriwa ni tangazo la ZEC kuhusu tarehe ya uchaguzi huo.

Balozi Iddi aliyasema hayo jana alipofanya mkutano na waandishi wa habari na kuongeza kuwa bajeti ya uchaguzi wa marudio haitatofautiana na bajeti ya uchaguzi uliopita ambayo ilikuwa takribani shilingi bilioni 7.

Hivi karibuni, Chama Cha Wananchi (CUF) kupitia Kaimu Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Jussa Ismail Jussa, walipinga taarifa iliyotolewa na Kamati maalum ya CCM kuwa kwa mujibu wa mazungumzo yanayoendelea uchaguzi utarudiwa. CUF walisisitiza kuwa hakutakuwa na uchaguzi wa marudio na badala yake wataendelea kumlinda mshindi halali wa matokeo ya uchaguzi huo.

Zari: Tiffah Ni Rais Wenu ajaye
Meya auawa Siku Moja baada ya Kula Kiapo