Mtangazaji wa kipindi cha Super mix ya East Afrika radio na Mchekeshaji ‘Zembwela’ ametoa ya Moyoni na kusema anakerwa sana na mabinti ambao wanapiga picha za utupu na kuziweka mitandaoni .

Zembwela amezugumza hayo leo wakati anafunga kipindi cha super Mix akizitaka Ngo’s ambazo mbalimbali ¬†zinashuhulika na masula ya haki za binadamu kuwashtaki watu wa aina hiyo kwani wataharibu vizazi vijavyo ambavyo vitakuja kushuhudia picha za aina hizo.

”hivi kwa nini hawa watoto wasishtakiwe hata na haki za binadamu kwa sababu utakuta kapiga picha yake alafu ananitag ili nishuhudie kamba zake ambazo zimeshindwa kufunika makalio, wanasikistisha sana na sheria ya mitandao ifanye kazi”.

Aidha amesema kuwa mabinti hao wanajitafutia umaarufu kwa kujidhalilisha kwenye mitandao huku wakijisifu kuwa na wao ni mifano ambayo inapaswa kuchukuliwa na wengine.

Wengine wanasema wao ni marole model, sasa mtoto wangu naye ajifunze kuanika mwili usiokuwa na nguo? sijui wanajiita ambaer nanii mwingine anajiita pesa kwa kingereza ni vitoto vidogo sana.- alisema Zembwela akionesha kuwa anawafahamu hivyo katupa jiwe gizani.

Shomari Kapombe Aanza Kujifua Taratibu
Mario Gotze Kurejeshwa Westfalenstadion