Mahakama katika gereza lenye ulinzi mkali la Jangwani nchini Chad, imewahukumu watu 262 waliokamatwa wakati wa maandamano ya umwagaji damu ya kupinga utawala, kifungo cha miaka miwili hadi mitatu jela baada ya kusikilizwa kwa kesi hizo bila ya mawakili na vyombo vya habari.

Watu 80, kati ya watu 401 waliokuwa washtakiwa, wengi wao wakiwa waandamanaji vijana walipewa kifungo cha mwaka mmoja hadi miwili na 59 waliachiliwa huru, huku mwendesha mashtaka wa umma wa N’Djamena, Moussa Wade Djibrine, akithibitisha hukumu hiyo.

Gereza lenye ulinzi mkali la Jangwani nchini Chad. Picha ya Africanews.

Kesi hiyo, iliyodumu kwa siku nne ilirushwa na televisheni ya taifa pekee bila ya uwepo wa vyombo vingine vya habari, na mwendesha mashtaka hakutoa hukumu hiyo hadharani hadi siku tatu baadaye, aliporejea kutoka Ikulu.

Oktoba 20, 2022, karibu watu 50 wengi wao wakiwa waandamanaji vijana walipigwa risasi na kufariki huko jijini N’Djamena, wakati Polisi walipofyatua risasi kwenye jaribio dogo la kutawanya mkutano.

Jeshi, Viongozi wa kiraia wasaini makubaliano
Hatma ya Rais Ramaphosa mikononi mwa ANC