Sakata la upotevu wa makontena bandarini limeendelea kuchukua sura mpya ambapo sasa jeshi la polisi linawashikilia watu 40 wanaosadikika kuhusika na upotevu huo.

Kamanda wa Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa indadi hiyo inajumuisha watumishi wa TRA, watumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na wafanyakazi wa bandari kavu (ICD).

Kamanda Kova alifafanua kuwa sakata hilo sasa limechukua sura mpya kwani awali washikiliwa hao walikuwa na tuhuma lakini sasa baada ya uchunguzi wamebainika kuwa walihusika kwa namna moja au nyingine kula njama ya kutorosha makontena hayo yaliyokwepa kodi ya mabilioni.

Alisema kuwa kati ya watu hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo, 26 ni watumishi wa TRA na watatu ni wafanyakazi wa bandari kavu inayomilikiwa na kampuni ya Said Bakhresa ambaye ni mmiliki wa kituo cha runinga cha Azam TV.

Mwanamke Ahukumiwa Kupigwa Mawe hadi Kufa
Bodi Ya Ligi (TPLB) Kukutana Jumapili