Aliyekua meneja wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas, amedhamiria kumsajili kiungo kutoka nchini Nigeria Mikel John Obi itakapofika mwezi Januari mwaka 2017.

Andre Villas-Boas kwa sasa ni meneja wa klabu ya Shanghai SIPG inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini China.

Gazeti la The Daily Mirror limeeleza kuwa, meneja huyo kutoka nchini Ureno anaendelea kujipanga kuiwania saini ya Obi, ambaye pia yupo katika mikakati ya klabu ya Olympique Marseille ya nchini Ufaransa.

AVB ambaye amechukua nafasi ya Sven-Goran Eriksson tayari ameshawahakikishia viongozi wa klabu ya Shanghai SIPG kuhusu uwezekano kumsajili Obi, huku akiamini ukaribu uliopo kati yao utakua kigezo cha kufanikisha azma yake.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea, tangu utawala wa Antonio Conte ulipoanza kazi mwanzoni mwa msimu huu.

Tayari Obi ameshapewa ruhusa ya kusaka mahala pa kucheza soka lake kuanzia mwezi Januari mwaka 2017.

#HapoKale
Lwandamina Atambulishwa Rasmi Young Africans