Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ambwene Yesaya ‘AY’, amemtaja msanii wa R&B, Benard Paul ‘Ben pol’ kuwa ndiye mfalme wa muziki huo kwa Afrika Mashariki, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Afrika mashariki na kati.

Akizungumza Dar es salaam juzi, AY alienda mbali zaidi na kumfananisha Ben Pol na mkali wa R&B kutoka Marekani, R.Kelly na kusema ndiye R.Kelly wa Tanzania, hivyo tunapaswa kumpa ushirikiano.

Alisema msanii huyo akipewa ushirikiano atafanya mambo makubwa zaidi na kuiwakilisha nchi vizuri kupitia muziki anaoufanya.

”Nimefuatilia katika kazi zake nimegundua ni msanii aliye na kipaji kikubwa mfano mzuri wimbo wake wa ‘moyo mashine’ kafanya vizuri katika ile kazi,” alisema.

”Kusini mwa Jangwa la Sahara na Mashariki ya kati ndio R.Kelly wetu, sasa cha kufanya tuzidi kumuonesha ushirikiano wetu, ili azidi kufanya vizuri zaidi na kwamba hivi sasa ametoa wimbo wake wa ‘phone’ ambao amemshirikisha Mr Eazi,” alisema AY.

benpol21r-kelly-gq

 

 

Lowassa asikitishwa na Ukawa
Video: Watu 12 wafa ajali ya jahazi, Mtatiro, Lipumba waingia vita mpya...

Comments

comments