Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ambaye jana alikihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwenda UDP, ametoa msimamo wake kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mgombea urais wa Chama hicho, Edward Lowassa.

Ole Medeye alihama CCM mwaka 2015 akimfuata Lowassa aliyehamia Chadema na kupewa nafasi ya kugombea urais, akiwa ni mtu wake wa karibu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujiunga na UDP jijini Dar es Salaam, Ole Medeye alisema kuwa urafiki wake na Lowassa hauwezi kutenganishwa na siasa.

“Lowassa ni kama ndugu yangu na rafiki yangu hivyo kuhama kwangu Chadema hakutaathiri umoja na ukaribu wetu. Siwezi kujitenganisha naye kwasababu ya siasa,” Medeye anakaririwa.

Ole Medeye alieleza kuwa ameamua kuihama Chadema kwa sababu anataka demokrasia ya kweli huku akipinga mwenendo wa chama hicho dhidi ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson.

 

Ole Sendeka kutaja orodha ya viongozi wa Upinzani ‘Mafisadi wa Mafuta’
Jeshi la Polisi lamsaka Zitto, lazima kongamano la ACT- Wazalendo