Timu ya Biashara United Mara imeizima Al Ahly Tripoli ya Libya katika mchezo wa Mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho hatua ya awali, uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Biashara United Mara inayoshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo inayoratibiwa na Shirikisho la soka Barani Afrika ‘CAF’, imeonesha kiwango safi ambacho kimechochea upatikanaji wa ushindi wa mabao 2-0.

Bao la kwanza la Biashara United Mara lilipatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa Deogratis Judica Mafiye kabla ya Atupele Green hajafunga bao safi kipindi cha pili.

Kwa ushindi huo Biashara United inapaswa kujiandaa kikamilifu kabla ya mchezo wa Mkondo wa pili utakaounguruma mjini Tripoli, Libya siku ya Jumamosi (Oktoba 23).

Al Ahly Tripoli itapaswa kusaka ushindi wa zaidi ya mabao mawili kwa sifuri ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, huku Biashara United itahitaji matokeo ya sare ama ushindi ili kuendelea na safari ya kusaka hatua ya Makundi.

Didier Gomes: Nimewasoma vizuri Jwaneng Galaxy
Neema yawashukia wakazi wa Siha