Sentahafu wa Manchester United, Chris Smalling amefichua kuwa beki kinda wa klabu hiyo, Cameron Borthwick-Jackson atakuwa suluhisho la safu ya ulinzi Old Trafford.

Borthwick-Jackson mwenye umri wa miaka 18, alitokea benchi na kuchukua nafasi ya Ashley Young  aliyeumia muda mfupi kabla ya mapumziko na kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Ni mchezo wa sita wa ligi kwa kinda huyu wa kutoka academy ya United tangu alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya West Brom mwezi Novemba mwaka jana.

Smalling ambaye nae aling’ara sana kwenye mchezo dhidi ya Liverpool, amesema: “Nadhani ameonyesha kuwa yupo tayari kwa kucheza katika mechi za kimashindano, alionyesha kiwango cha hali ya ju. Kung’ara sehemu kama Anfield kunathibitisha kuwa atang’ara kwingineko kokote kule

Mkwasa Ashangazwa Na Maamuzi Ya Nadir Haroub Cannavaro
Stand Utd Waikana Safari Ya Chanongo Na Ubwa