Beki na Nahodha Msaidizi wa KMC FC, Andrew Vicent ‘Dante’ amesema mechi zilizosalia ni lazima wapambane kuhakikisha wanapata alama tatu kwani ndizo zitaamua hatma yao kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

KMC FC inashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 29, ikicheza michezo 28 , huku ikibaki za mechi zote ugenini dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Dante amesema mechi hizo ni muhimu kwao kwani kama wakipata pointi sita watakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya sasa kutokana na tofauti ya pointi zilivyo na huku ikiombea nyingine kupoteza.

“Muhimu kushinda kwenye mechi hizi ili kuepuka suala la kushuka daraja, tunajua tuna mechi ngumu mbele yetu lakini lolote lile zuri linaweza kutokea kwa sababu huu ni mpira”

“Wachezaji wote tupo kwenye morali nzuri kuhakikisha tunapata pointi kwenye mechi hizi na sio kufungwa, suala la kushuka daraja hatutaki litokee kabisa kwetu.” Amesema Dante

KMC itakuwa ugenini dhidi ya Prisons Juni 06 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya kisha mchezo wake wa pili huko huko ugenini itacheza dhidi ya Mbeya City siku tatu baadae.

Magonjwa ya mlipuko: Elimu ya afya ni muhimu kwa jamii
Serikali kuja na mpango maalum ufugaji wa Samaki