Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumpata Diwani wa Kata ya Kawe (CCM), Mutta Rwakatare (43) aliyekuwa akitafutwa na ndugu zake kuanzia Februari mwaka huu kwa madai amepotea.

Kamanda Muliro amesema baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi limefanikiwa kumpata Mutta Rwakatare jana Jumatatu (Mei 23) maeneo ya Tabata akiwa katika nyumba ya mwanamke mmoja aitwaye Ashura ambaye amedai ni rafiki yake wa siku nyingi.

Kamnda Murilo amesema Mutta alifika kwa Ashura Mei 19 mwaka huu akiwa katika hali ya ulevi uliopindukia.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa, Kutokana na mazingira ya ulevi ambayo Diwani huyo amekutwa nayo na maombi yaliyotolewa na ndugu zake kwa Jeshi hilo kwa ajili ya matibabu, ndugu pia walitoa kumbukumbu za nyuma, mwenendo na tabia za ndugu yao.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limekabidhi Diwani huyo kwa ndugu zake kwa ajili ya kufanyiwa na kupewa ushauri wa Kisaikolojia

Juma lililopita Meya wa Manispaa Kinondoni, Songoro Mnyonge akiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani aliviomba Vyombo vya Dola, Wanahabari kusaidia kumtafuta Diwani huyo ambaye ni mtoto wa marehemu Dk Getrude Rwakatare.

Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Jiji la Arusha
Rais Samia atajwa kati ya watu 100 wenye ushawishi duniani