Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge Arusha Mjini ila anachofanya sasa ni kutekeleza ahadi za Rais Dkt. John Magufuli za kutatua kero za wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari, ambapo amesema kuwa taarifa zinazosambazwa kuwa atagombea ubunge jimbo la Arusha mjini ni za wanasiasa wasiojiamini na wameshindwa kutatua kero za wananchi.

Amesema kuwa baadhi wabunge hawaonekani majimboni na kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi zilizopaswa kufanywa na wabunge hao hivyo kuwa na hofu kubwa kuwa wanaweza kupokonywa nafasi zao.

“Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo ya kisiasa, sisi tunachapa kazi, huu ni muda wa kazi hatufanyi siasa,”amesema Gambo

Hata hivyo, Gambo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza katika shughuli ya uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa.

Yanga yaichapa Kagera, ni zamu ya Simba na Mtibwa leo
Hamisa Mobetto aitafuta amani kwa Zari