Katika kuunga mkono ukuaji wa fani mbalimbali nchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), imejitosa kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa wanajiolojia wa Tanzania unaofanyika mkoani Arusha wa (Oktoba 4-7, 2022) ulionaratibiwa na Chama cha Watalaamwa Jiolojia Tanzania (TGS), wenye wanachama zaidi ya 300.

Mrakibu waJiolojia katika Kampuni ya GGML, Eric Kalondwa amesema kampuni hiyo imedhamini mkutano huo kwa shilingi milioni 25 uliofunguliwa na Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko kwa niaba ya Makamuwa Rais, Dkt. Philip Mpango na ukitarajiwa kufungwa na Waziri wa Maji, Juma Aweso.

Amesema, katika mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kwenye mikoa tofauti, jumla ya wanajiolojia 11 kutoka mkoani Geita wameshiriki na kwamba umelenga kubadilishana uzoefu wa progamu mbalimbali za kuwaweka pamoja watu wenye fani zinazofanana huku wanajiolojia wa GGML wakifaidika na mambo mengi tangu kunzishwa kwa chama hicho.

“Mkutano wa mwaka huu unalengakukazia suala la upatikanaji wa bodi yawanajiolojia hasa ikizingatiwa fani hiyoinajumuisha watu kutoka maeneo mbalimbaliikiwamo wanaofanya kazi kwenye uchimbaji wamafuta, kwenye maji, madini ya aina mbalimbalitofauti na na dhahabu,” amesema Kandolwa.

Hata hivyo, amekiri uwepo wa changamoto ya uhaba wa wanawake kusomea fani hiyo na kusema, “GGML inafanya vizuri kuendeleza wanajiolojia toka wanapokuja kujifunza kwa vitendo na wanaokuja kazini, wanaopitia kwenye mgodi wetu wanasifu kwa mapokeo makubwa tunayowapa kulingana na program ya mwaka tuyonawaandalia.”

Awali, akifungua mkutano huo Waziri wa madiniDk. Biteko alisema wizara iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wakuanzishwa kwa bodi ya wanajiolojia na kusema Serikali itatoa nafasi kwa wadau kutoa maoni kuhusu muundo wa bodi, usimamizi wake, upataji wa vyanzo vya fedha na uangaliaji wa mambo ya kisheria.

Amesema, wakati Serikali inakamalimisha mchakato wa kuundwa kwa bodi, ni muhimu wajiolojia kuhakikisha wanaiendeleza taaluma yao ili kuipatia nchi heshima ikiwemo kuwapa wawezekaji taarifa sahihi ili kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya Madini huku akiwataka Wajiolojia kuheshimisha taaluma yao.

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wataalam wajilojiaTanzania, Prof. Abdulkarim Mruma aliieleza hadhira kuhusu utajiri wa kijiolojia ambao nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa nao, na kuelelezea namna bora ya kuitumia taaluma hiyo kwa maendeleo ya nchi na jamii nzima kiujumla.

Bigirimana awaita mashabiki Kwa Mkapa
Nasredine Nabi: Hata sisi tunawafahamu vizuri