Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya klabu ya Simba SC Haji Sunday Manara, amempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuonyesha matumaini ya kurejesha ligi kuu pamoja na michezo mingine.

Rais Magufuli amezidi kuleta matumaini ya kurejea kwa michezo nchini baada ya kusema anatarajia kuruhusui sekta hiyo kurejea kuanzia wiki hii endapo idadi ya  wagonjwa wa virusi vya corona itaendelea kupungua.


Rais Magufuli alisema hayo jana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato Mkoani Geita. kasi ya maambukizi imeshuka na idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa, hivyo anafikiria kufungua vyuo na kuruhusu michezo endapo hali itaendelea kuwa hivyo hadi wiki ijayo.

Manara amesema endapo ligi itaendelea na Simba ikatimiza lengo la kutwaa ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya tatu mfululizo, uongozi wa klabu hiyo hautosita kumkabidhi kombe Rais Magufuli, endapo itampendeza kufanya hivyo.

“Kwanza tumshukuru Mh. Rais kwa maono yake kwa maelezo yake, kwa kweli hii kwetu sisi hususani wana Msimbazi limetufariji sana. Kwa sababu TFF ilikuwa iko katika kona mbaya safari hii, kwa misingi ya Utanzania wetu ilikuwa imekaa kwenye hata kama hawajasema.”

“Mnajua Watanzania na wanahabari, tunahitaji points chache mnoo ili kuwa Mabingwa, tutauchua hakuna ambaye anahoji hilo jambo.”

Lakini Haji Manara amesitiza kuwa tahadhari iendelee kuchuliwa na isije ikatafrisiliwa vibaya baada ya hotuba ya Mh. Rais, lakini akamalizia na dongo hili hapa.

“Kwa kuwa Mh. Rais ndiye aliyeagiza ligi irudi hatuna ubaya wala si dhambi ukizingatia kombe hili la tatu mfurulizo, maanake ni letu yaani “TFF” hawatapata kombe tena ni mali yetu, tutampelekea hata Mh. Rais ikimpendeza akae nalo ikibidi likae ikulu na akaona vipi likae Magogoni si mbaya wala si dhambi, kombe hili ni la Simba na Simba tumelichukua moja kwa moja kumpa tunu ile Raisi wetu tutapungukiwa nini sisi.”

“Nitawaomba viongozi, nitamuomba C.E.O aweke pendekezo kwenye bodi ikipendeza raisi akae nalo hili kombe liwe kumbukumbu kwasababu yeye ndo amerejesha hii ligi bila hivyo hapa kungekuwa na mkanganyiko mkubwa hapa kama baadhi ya Nchi zilivyo,”

“Sasa lazima umpe zawadi na zawadi gani zaidi ya kikombe ambacho sisi tumekichukua moja kwa moha, sisi tuna vingine vingi, tuna makombe 54 kabatini kumpa hili moja Raisi wetu kuna shida gani”:- Haji Manara

Mbunge Lijualikali amwaga machozi Bungeni aomba kuhamia CCM
Balinya afichua kilichomuondoa Young Africans