(i) Kuanza ujenzi wa miradi saba (7) ya barabara yenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineeering Procurement Construction and Finance ( EPC + F).

(ii) Kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara kutoka Kibaha – Chalinze – Morogoro Expressway yenye urefu wa kilometa 205 kwa kutumia utaratibu wa kushirikisha Sekta Binafsi (Public Private Partnership – PPP).

(iii) Kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa ya barabara katika maeneo mbalimbali yenye jumla ya urefu wa kilometa 1,031.98.

(iv) Kuendelea na Miradi ya Ujenzi wa Barabara iliyosaniwa Katika Mwaka wa Fedha 2022/23 yenye jumla ya urefu wa kilometa 393.6

(v) Kuendelea na ujenzi wa madaraja makubwa mawili (2) ya JPM (Kigongo – Busisi, Mwanza) na Pangani (Tanga) pamoja na kujenga madaraja mengine katika maeneo mbalimbali nchini.

(vi)Kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 269.12 ambazo zinatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2022/23.

(vii) Kuendelea na utekelezaji wa mradi ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Msalato pamoja na Kuendelea na kazi za ukarabati na upanuzi wa viwanja vingine vya ndege katika mikoa mbalimbali.

Moses Phiri apewa dozi maalum Simba SC
Marcus Rashford kusaini mkataba mpya Man Utd