Hujaji wa mmoja wa Nigeria, Hajat Aisha Ahmed, amefariki dunia mjini Makka, Saudi Arabia kufuatia kupata maradhi ya ugonjwa ambao haukujulikana.

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ustawi wa Mahujaji wa Jimbo la Nasarawa, Idris Al-Makura amesema Aisha Ahmed anayetoka eneo la Serikali ya Mtaa wa Keffi jimboni humo, alifariki siku ya Jumatano Juni 29, 2022 baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Al-Makura, amewaambia waandishi wa Habari mjini Makka, Saudi Arabia kwamba, marehemu hakuwa na rekodi ya kuugua kabla ya kuondoka nchini Nigeria.

“Marehemu hakuwa na historia ya wowote wala kuripotiwa kuwa na ratiba ya matibabu wakati wa kuondoka kwenye Ardhi Tukufu na tulikuwa pamoja Madinah licha ya kwamba baadhi ya mahujaji waliugua siku mbili zilizopita,” amesema Al-Makura.

Katibu huyo Mtendaji Amesema, “Mara ya kwanza alipelekwa katika Hospitali ya Tume ya Kitaifa ya Hajj huko Makka na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya King Abdulaziz ambako alifariki na tayari tumeiarifu familia yake ipasavyo juu ya kifo hicho.”

Familia ya marehemu Aisha Ahmed, imetumiwa rekodi ya video inayoonesha mchakato wa kuthibitishwa kifo chake, ikiwemo taratibu za mazishi na hatimaye, maziko.

Ujenzi miradi ya kimaendeleo wapongezwa
Mgogoro wa mpaka wazusha mapigano