Kiungo wa Manchester United Juan Mata alisafirisha kundi la watoto maskini ambao wanacheza soka kutoka India na kuwaleta Uingereza ili kuuona uwanja wa Old Traford na kupiga picha katika maeneo mbali mbali ya uwanja huo na kujifunza kuhusu soka.

Ziara ya watoto hawa inakuja baada ya miezi michache iliyopita kiungo huyo kutembelea mji wa Mumbai na kuona mazingira magumu wanayoishi watoto hawa na ndipo aliamua kuwaleta jijini Manchester kama njia ya kuwahamasisha kufikia malengo yao.

Mata ameamua kuwasaidia watoto hawa kwa kuwahamasisha kuhusu kucheza soka lakini pia kuwapa elimu ya maisha na darasani mpango ambao tayari baadhi ya nyota wakubwa duniani wameanza kumuunga mkono.

Juan Mata aliwaalika Ander Herrera na nyota wa zamani wa United anayekipiga Everton Morgan Schnerdelin kujumuika pamoja na watoto hao pamoja na kupiga nao picha kabla ya kuwapeleka katikati ya uwanja wa Old Traford.

Katika kuendeleza suala hilo Juan Mata amewaomba wacheza soka wenzake kuchangia hata 1% ya kipato chao ili kuwasaidia watoto wasio na uwezo huku akisema anaaamini wachezaji wenzake wa Manchester United watamuunga mkono.

Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini amemtumia Juan Mata salamu za kumuunga mkono kwa kile anachokifanya huku pia Mats Hummels wa Bayern Munich, Serge Gnabry wa Hoffnheim  nao wakiunga mkono kampeni hii ya Juan Mata.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 14, 2017
Zari aibua maswali baada ya kutua Bongo

Comments

comments