Mwandishi wa habari Erick Kabendera leo ametuma salamu kwa waombolezaji wa msiba wa mama yake ikiwa ni siku ambayo mama yake ameagwa kwenye kanisa katoliki la Mt. Francis Xavier Chang’ombe Jijini Dar es salaam.

Hayo yamejiri baada ya jana Alhamisi, maombi ya Kabendera ya kuhudhuria ibada ya kuaga mwili wa mama yake, Verdiana  kugonga mwamba baada ya Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuyatupilia mbali maombi hayo.

Salamu za Kabendera zilizosomwa kanisani hapo na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alizopewa na mwanasheria wa kabendera Jebra Kambole. Ambayo ni barua iliyoandikwa kama ifuatavyo.

Kuna mama mmoja,

Anafariki mara moja,

msiba mara moja,

Uchungu wa kuondokewa na mama ni mkuwa sana, hasa anapokuwa ameondoka na umeshindwa kumuaga kama ilivyotokea kwangu.

Hata hivyo nimefarijika kwa watanzania wote walioguswa na msiba huu bila kujali itikadi zao za kisiasa na kidini na kunisaidia kumsitiri mama yangu.

Upendo huu umeonyesha nchi ambayo nimeipenda na naipenda kutoka moyoni. shukurani za dhati ziwafikie watu wote kwa upendo wao na ushiriki wao kufanikisha msiba wa mama yangu.

Mwenyezi Mungu na awabariki sana na kuwaongezea pale mlipopunguza kwa ajili yangu mtuombee.

Awali wakati wa kusoma barua hiyo, Kabwe alianza kwa kuwasomea waombolezaji salamu za wakili wa Kabendera, Kambole aliyesema ” siku hizi tatu zimekuwa ngumu sana kwa Erick, katika jambo gumu ambalo nimewahi kulifanya kama mwanasheria ni hili la kumpelekea Erick taarifa za kufiwa na mama yake.”

Video: Ujumbe wa Kabendera kutoka gerezani, Mauaji, ukatili watanda mwaka mpya
Marekani yaagiza wananchi wake kuondoka Iraq

Comments

comments