Ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40 umekumba wakulima kote Afrika Mashariki, na kusababisha uhaba wa chakula na kutishia njaa ambapo nchini Kenya, ardhi ya kilimo katika eneo lililo nje kidogo ya mji mkuu wa Nairobi, inaandaliwa ili iweze kuwa na rutuba.

Hata hivyo, kukosekana kwa mvua kwa misimu minne imebadilisha maisha ya mkulima Alice Muthoni ambaye anasema ni takriban imepita miaka mitatu tangu apate mavuno mengi na miaka iliyosalia hali ilikuwa ni ya kusikitisha.

Amesema, ekari moja ya mahindi kwa kipindi ambacho hali ya ukame ilitawala ilikuwa ikitoa gunia la mahindi, ambalo liliweza kutosheleza upatikanaji wa chakula pekee, na hivi majuzi Kenya ilisema inaondoa marufuku ya miaka kumi ya kulima na kuagiza hadharani viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMO).

Mmoja wa Wakulima wa Mahindi akiwa Shambani. Picha ya CIMMYT.

Hatua hiyo, imekuja huku kukiwa na shinikizo kutoka kwa serikali ya Marekani, ambayo ilikuwa imesema kuwa marufuku hiyo iliathiri mauzo ya nje ya kilimo ya Marekani na msaada wa chakula ambapo katika kukabiliana na janga la ukame matumizi ya mazao yaliyobadilishwa vinasaba yanaonekana kama suluhu.

Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama wa Mazingira ya Kenya (NBA), Roy Mugiira amesema wamekuwa wakifanya majaribio ya aina moja ya mahindi ambayo yamebadilishwa vinasaba (GM), ili kukabiliana na ukame ambayo yanaweza kusababisha mavuno wakati wa shida ya maji na wakati wa vipindi vya ukosefu wa mvua.

Hata hivyo, Mamlaka za usalama wa chakula, haki za walaji na makundi ya viumbe hai wamelaani kuondolewa kwa marufuku hiyo, wakisema kungekuwa na mashauriano ya umma kuhusu suala muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi na kusema uamuzi huo unaminya uhuru wa Wakenya kuchagua kile wanachotaka kula.

Waandamanaji wahukumiwa kifo Iran
Majeraha ya Nkunku yampeleka Randal Kolo QATAR