Kesi mbili zimewasilishwa katika mahakama ya juu nchini Kenya, zikitaka kufutwa kwa ushindi wa Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kufuatia uchaguzi wa tarehe 26 mwezi Oktoba kufanyika huku wapinzani wakiwa wamesusa kushiriki.

Kesi hizo zimewasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa kilome, Harun Mwau na mawakili Njonjo Mue na Khelef Khalifa, ambapo wanasema kuwa katiba ilikiukwa wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.

Aidha, Kesi ya Mwau ambayo inawashtaki IEBC, mwenyekiti wake na Rais Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba, inasema kuwa kushindwa kwa IEBC kuruhusu vyama kuandaa uchaguzi, kuliwanyima haki wale ambao walitaka kugombea.

Hata hivyo, kwa upande wa Kesi iliyowasilishwa na mawakili, Mue na Khalifa nayo kwa upande mwingine inazungumzia ukiukwaji wa katiba ikiwemo kuchapisha picha za watu wasiostahili kwenye makaratasi ya kupigia kura akiwemo mgombea wa muungano wa NASA Raila Odinga, ambaye alikuwa ametangaza kuwa hangegombea nafasi ya urais

Dawa za kusisimua misuli zamponza mwanariadha Kenya
Neymar kuwa mrithi wa Ronaldo?