Wanafunzi wapatao  646,148 wamesajiliwa kufanya upimaji wa kitaifa wa mitihani ya kidato cha pili kwa mwaka 2020, ambayo imeanza leo Novemba 9 Tanzania bara na itamalizika Novemba 20.

Kwa Mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde, akitangaza kukamilika kwa maandalizi ya mitihani hiyo, amesema kuwa kati ya watahiniwa hao, wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana ni 344,317 sawa na asilimia 53.29. 

Dkt. Msonde amewaonya wasimamizi wote pamoja na kamati zinazosimamia kuzuia mianya yoyote inayoweza kuharibu matokeo kutokana na udanganyifu na kuwataka kuzingatia miongozo iliyotolewa Baraza la Mitihani.

“Baraza halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kujihusisha au kusababisha udanganyifu kutokea katika upimaji mitihani”, amesema Dkt. Msonde

Aidha, ameeleza kuwa Mitihani ya Darasa la Nne itafanyika Novemba 25 na 26, ambapo idadi ya Wanafunzi waliosajiliwa ni 1,825,679 wakiwemo Wavulana 909,068 na Wasichana 916,611.

Diwani mteule wa CCM afariki kwa moto
Thamani ya 'Triple C' ni Bilioni 2, hang'oki Msimbazi