Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa mjumbe mpya maalum wa Umoja wa Afrika (AU) kwenda nchini Libya akichukua nafasi ya Dileita Mohamed Dileita wa Djibouti aliyeishika nafasi hiyo tangu mwaka 2014.

Uteuzi huo uliofanywa na Umoja wa Afrika katika kikao chake kilichofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kimeuelezea kuwa sehemu ya juhudi za Umoja huo katika kuhakikisha inarudisha hali ya usalama na amani nchini Libya.

Kamishna wa Amani na Usalama wa AU, Smail Chergui jana alitangaza uteuzi huo alipokuwa anatoa muhtasari wa majadiliano na makubaliano ya kikao hicho killichowakutanisha viongozi wa ngazi za juu wa nchi wanachama.

Libya imekuwa katika machafuko tangu kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi.

Ma-MC, Wapishi, Kumbi za Harusi kuanza kulipa kodi
Picha: Madaktari wafanikiwa kuwatenganisha mapacha waliozaliwa wameungana