Imefahamika kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans Mohamed Nasrdeen Nabi amekuwa kikwazo cha timu hiyo kushindwa kuongea na waandishi wa habari kama kanuni za mashindano ya Kombe la Shirikisho zinavyoagiza.

Young Africans walipaswa kuwakilishwa na Kocha Nabi na Nahodha kwenye mkutano ba waandishi wa habari uliokuwa umepangwa kufanyika saa tano na nusu asubuhi, kwenye chumba cha Mikutano cha Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Kocha Nabi alilazimika kusitisha mpango huo kufuatia kazi kubwa aliyokua nayo ya program za luninga kuelekea mchezo wa kesho Jumapili (Julai 25) dhidi ya Simba SC.

Taatifa hizo zimeongeza kuwa baada ya Kocha Nabi kupotezea Mkutano na waandishi wa habari, ameuthibitishia uongozi kuwa endapo TFF itawaadhibu kwa kuwatoza faini kwa kosa hilo, kocha huyo amesema atalipa yeye.

Awali Afisa Habari na Mahusiano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo alisema kuwa, sababu ya klabu ya Young Africans kufutiwa kuzungumza na Wanahabari saa tano na nusu asubuhi ya leo imesababishwa na kocha mkuu wa kikosi hicho, Mtunisia, Mohamed Nasrdeen Nabi na nahodha wake kushindwa kuhudhuria tukio hilo na badala yake kuhudhuriwa na kocha wa makipa, Mkenya Razak Siwa na Meneja wa timu hiyo Hafidh Swalehe ambao hawakuruhusiwa kuendelea na mahojiano hayo.

Mo kuvunja ukimya Simba SC
Coastal Union, Mtibwa Sugar zapeta Ligi Kuu 2021-22