Katika hali ambayo wengi hawakuitarajia, mgombea urais wa serikali ya Mapinduzi, Zanzibar Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amejitoa hadharani na kutangaza matokeo yanayoonesha kuwa ameshinda nafasi ya urais.

Mgombea huyo amefanya mkutano na vyombo vya habari mapema leo asubuhi na kuonesha kueleza kuwa kwa mujibu wa matokeo yaliyokusanywa kwenye vituo kupitia fomu maalum za Tume ya Taifa ya Zanzibar (NEC), anaongoza kwa kura 200,007 huku mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Ali Mohamed Shein akipata kura 178,363.

Aliwataka ZEC kutangaza matokeo hayo kama yalivyo bila kubadili takwimu hizo alizodai ni halali kwa mujibu wa fomu zilizobandikwa vituoni.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ZEC, ni Tume hiyo pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya urais. Bado Tume hiyo inaendelea kutangaza matokeo kutoka katika majimbo mbalimbali.

Davido, Swizz Beatz, Neyo Wampa Shavu Diamond Kiroho Safi
Matokeo Rasmi: Magufuli Aongoza Majimbo Matatu Ya Awali