Rais John Magufuli amefuta hati ya ardhi yenye ukubwa wa hekari 1870 iliyokuwa inamilikiwa na mwekezaji, Kapunga Rice Project Limited.

Kutokana na uamuzi huo wa rais, hivi sasa ardhi hiyo ni mali ya umma itakayotumiwa na wanakijiji wa Kapunga.

Akitangaza uamuzi huo wa rais, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema kuwa rais amechukua uamuzi huo ili kuondoa mgogoro wa ardhi kati ya mwekezaji huyo na wananchi. Alisema kuwa ardhi hiyo ni zawadi ya kwanza ya rais kwa wananchi.

Waziri Lukuvi alimuagiza Mkuu wa Mkoa kuandaa orodha ya watu wanaomiliki mashamba ambayo hawajayaendeleza ingawa wanapata mikopo mbalimbali kupitia hati za mashamba hayo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapunga, Brighton Mwinuka aliishukuru serikali kwa uamuzi huo na kueleza kuwa hivi sasa kijiji hicho kitakuwa na uwezo wa kuendelea na mipango ya maendeleo.

Naye meneja mradi wa Kampunga Project, Sumil Tayic alisema kuwa uongozi wa Kampunga Rice Prroject Limited wamekubaliana na uamuzi wa rais na kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi hao.

Kijiji cha Kapunga kinakadiriwa kuwa na wananchi takribani 4500.

Bahanuzi Aiweka Pazuri Mtibwa Sugar Mapinduzi Cup
Ubishi Kumalizwa Kisiwani Unguja, Ni Dhambi Mtoto Kutumwa Sokoni