Majina ya baadhi ya wanafamilia waliofariki dunia katika ajali iliyotokea Korogwe mkoani Tanga na kusababisha vifo vya watu 17 yametolewa na Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga, Dkt. Salma Sued.

Dkt. Salma amesema, waliofariki ambao ni wanafamilia na kutaja majina yao kuwa ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema, Godwin Mrema, Yusuph Saimon na Zawadi Mrema.

Wengine ni Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina Lamosa, Evelina na Cosmas Mrema ambao kwa pamoja walifariki baada ya Basi dogo la abiria kugongana na Lori eneo la Magira Gereza lililopo tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, Tanga.

Idadi hiyo ya marehemu, inahusisha wanafamilia 14 na majeruhi 12 na wote walikuwa wakisafirisha mwili wa marehemu kwenda Moshi, Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi wakitokea Mkoani Dar es Salaam ambapo chanzo cha ajali ni mwendokasi na uzembe wa dereva wa Lori.

Lissu: Risasi zimempa maisha Dereva wangu
147 JKT wakutwa na VVU