Meneja mpya wa klabu ya Everton, Ronald Koeman ameanza mkakati wa usajili klabuni hapo kwa kutoa msukumo wa kuona mshambuliaji kutoka nchini Cameroon na klabu ya FC Porto, Vincent Aboubakar anaelekea Goodson Park wakati wa majira ya kiangazi.

Koeman aliyekabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Everton juma lililopita, ameelekeza nguvu zake kwa mshambuliaji huyo, kutokana na kuamini atakuwa mbadala mzuri wa Lomelo Lukaku, endapo itatokea anaondoka.

Lukaku anahusishwa na mipango ya kutaka kuihama Everton, na tayari mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wamejizatiti kumsajili.

Thamani ya Aboubakar mwenye umri wa miaka 24, inatajwa kuwa ni pauni milioni 16.

Aboubakar alijiunga na FC Porto, akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Lorient, mwaka 2014, na msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 18 kwenye michuano yote aliyocheza huko nchini Ureno.

Hans Poppe: Yanga Wanajifanya Wanajua Kila Kitu
Watatu Wakatwa Uchaguzi Mkuu Stand Utd