Wananchi wa Kijiji cha Engaruka Juu Wilayani Monduli, wanadaiwa kuwashambulia Viongozi wanane wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Engaruka iliyopo Mkoani Arusha kutokana na hasira walizokuwa nazo kwa madai ya kuuzwa kwa ardhi ya kijiji chao kinyemela.

Tukio hilo limetokea wakati viongozi hao ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa ya chama hicho walipokwenda kijijini hapo kufuatilia tuhuma za Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahamu Logolie kudaiwa kuuza ardhi ya eneo hilo.

Majeraha ya mashambulizi. Picha na Mwananchi.

Inadaiwa kuwa, mara baada ya kufika katika kijiji hicho kilichopo takriban kilomita 60 kutoka Monduli Mjini, walivamiwa na kundi la vijana wa kimasai maarufu kama morani zaidi ya 30 waliokuwa wamejikusanya na kuwashambulia.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe amesema miongoni mwa viongozi walioshambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Leliya Sengeita pamoja na Katibu wake, Joseph Namoyo na kudai kuwa uchunguzi juu ya tukio hilo umeanza.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 13, 2023
Habari Picha: Buriani Mama Sabina Lumwe