Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kuwa hoja zilizotolewa na wananchi na viongozi mbalimbali za kusitisha upandaji bei za umeme kwa wateja wa kati ni ngumu na zinahitaji muda kuweza kuzijadili

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, amesema kuwa kutokana na shirika hilo kuwajali wateja wa kipato cha chini, wateja hao hawataathirika na mapendekezo ya bei mpya na badala yake watabakia na bei iliyopo sasa.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni wiki moja tu kupita tangu Tanesco ilipo wasilisha maombi ya kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 18.19 kwa Ewura kwa mwaka 2017. ingawa siku chache zilizopita kwenye uzinduzi wa mradi wa kuboresha huduma za umeme kwa mkoa wa Dar es salaam, ambapo Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo  alisema hategemei tena kuona umeme ukipanda bei.

Mramba amesisitiza kuwa shirika hilo halina mpango wa kurudisha tozo ya kuunganishiwa umeme ya Sh 5,000 na gharama ya huduma kwa kila mwezi ya Sh 5,520 ambazo ziliondolewa mwezi Aprili mwaka huu.

“Tanesco ilitakiwa kufanya tathmini ya gharama za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme na kupeleka mapendekezo hayo Ewura, ili kupitiwa na wadau, sasa suala la kupanda au kushuka kwa bei itategemea na mapitio ya tathmini ya gharama za kuzalisha, kusafirisha na kusambaza tulizowasilisha Ewura,” alisema Mramba.

Bashe adai Lowassa alionewa CCM, aeleza uhusiano wao kwa sasa
Makonda kuiombea Kigamboni jengo lililoachwa na Hayati Aboud Jumbe