Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo amepokea mbio maalum za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Ndege wa Mwl JK Nyerere Terminal 1 ukitokea Mkoa wa Pwani.

RC Makalla amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa KM 355.6 ukizindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya Maendeleo ipatayo 46 iliyokamilika na iliyoko katika hatua za utekelezaji yenye thamani zaidi ya Bilioni 105.

Baada ya kukimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Agosti 23, 2021 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa katika Mkoa wa Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla.

Mkimbiza Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 kitaifa (kulia) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar.

Wakuu wa Nchi za SADC wahitimisha mkutano kwa kishindo
BASATA yakubali mwongozo mpya wa Maadili