Ripoti ya Dunia ya Furaha ya 2023, ambayo ilirekodi wastani wa kuridhika ulimwenguni na inasema azimio la mwanadamu la kuwa na furaha limekuwa ni la kustahimili na lenye hali ya kushangaza, kutoka kwa zaidi ya nchi 150, na Taifa la Finland lipo katika nafasi ya kwanza kwa mwaka wa sita mfululizo.

Viwango vya Ripoti ya Dunia vya Furaha kwa kiasi kikubwa vinatokana na tathmini za maisha kutoka katika upiogaji wa Kura ya Dunia, ya Gallup huku vigezo sita muhimu vinavyokadiriwa ni mapato (GDP per capita), usaidizi wa kijamii, umri wa kuishi kiafya, uhuru wa kufanya maamuzi ya maisha, ukarimu, na mauala ya rushwa.

Moja kati ya maswali ya kawaida la kupima ustawi wa watu ni – “Kwa ujumla, umeridhikaje na maisha yako ya sasa? na majibu hutegemea kipimo cha 0-10 (0 iokimaanisha kutoridhika kabisa, 10 ikiwakilisha kuridhika kabisa).

Matokeo ya kila mwaka ya ripoti daima hutegemea wastani wa tathmini za maisha katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ikihusisha ukosefu wa usawa wa furaha: Ni nchi gani ambazo hazikuwa na furaha zaidi, uwepo wa pengo kubwa kati ya nchi zenye furaha na zisizo na furaha katika orodha, huku nchi za juu zikiwa zimeunganishwa zaidi kuliko zile za chini.

Kwa nchi zilizo katika 10 bora, kwa mfano, alama za tathmini ya maisha ya kitaifa zina pengo la wastani la chini ya pointi 0.7. Katika 10 za chini, hata hivyo, anuwai ya alama inashughulikia alama 2.1 huku Afghanistan na Lebanon zikiwa nchi zisizo na furaha zenye wastani wa tathmini ya maisha zaidi ya pointi tano chini (kwa mizani inayoanzia 0 hadi 10) kuliko nchi kumi zenye furaha zaidi.

Nchi 10 za chini kabisa zisizo na furaha au kuwa na furaha kidogo ni :

  1. Zambia
  2. Tanzania
  3. Comoros
  4. Malawi
  5. Botswana
  6. Democratic Republic of Congo
  7. Zimbabwe
  8. Sierra Leone
  9. Lebanon
  10. Afghanistan

Kama ilivyo kwa Taifa la Ufini lililoongoza orodha kwa mwaka wa sita, sehemu kubwa ya waliobaki 10 bora bado haijabadilika huku Denmark ililinda nafasi yake ya pili, na Iceland ikishika nafasi ya tatu huku Taifa lililopaa juu katika viwango ni Israel iliyoshika nafasi ya nne, ikipanda kutoka nafasi tano kwa mwaka jana.

Nje ya 10 bora, Austria na Australia zilichukua nafasi za 11 na 12, ikifuatiwa na Canada, ambayo ilipanda nafasi mbili hadi ya 13 kutoka nafasi ya chini kabisa ya mwaka jana yaani ya 11 kwa kuwa na furaha zaidi na Ireland ilichukua nafasi ya 14 kwa kuwa Taifa lenye furaha zaidi, ikifuatiwa na Marekani (ya 15), Ujerumani (ya 16), Ubelgiji (ya 17), Cheki (ya 18), Uingereza (ya 19), na Lithuania (ya 20).

Mwaka baada ya mwaka, nchi zenye furaha zaidi huwa zile zile; kwa mfano, nchi 19 kati ya 20 bora za mwaka huu pia zilikuwa kwenye orodha mwaka jana, lakini kulikuwa na ubaguzi mmoja, Lithuania, ambayo imepaa kwa kasi zaidi ya miaka sita iliyopita, kutoka nafasi ya 52 mwaka 2017 hadi nafasi ya 20 kwa mwaka huu wa 2023.

Aidha, Ufaransa ilishuka kutoka 20 bora hadi nafasi ya 21 katika ripoti ya mwaka huu ambapo Mataifa 10 yaliyoshika nafasi 10 za juu kwa kuwa na furaha ni kama ifuatavyo,

  1. Finland
  2. Denmark
  3. Iceland
  4. Israel
  5. Netherlands
  6. Sweden
  7. Norway
  8. Switzerland
  9. Luxembourg
  10. New Zealand

Hata hivyo, mwandishi mwenza wa ripoti hii, Lara Aknin anasema Ripoti ya mwaka huu ina maarifa mengi ya kuvutia,na mojawapo inahusisha upendeleo wa kijamii.

Ripoti hiyo tayari ilikuwa imerekodi kuongezeka kwa ukarimu ulimwenguni kwa mwaka 2020 na 2021, kufuatia janga la Uviko 19. Na kulingana na data ya 2022, tabia ya watu kuwa wenye fadhila, ukarimu, na upendeleo kwa wengine ilikuwa ni asilimia 25 zaidi kuliko hapo awali.

Hali hii ya wema pia ilirekodiwa katika nchi kama vile Ukraine na Urusi. Mwaka 2020 na 2021, wote wawili walipata ongezeko la hisani ulimwenguni, wakati mwaka wa 2022, ufadhili ulikua kwa kasi nchini Ukraine na ulipungua nchini Urusi.

Hili linafurahisha, kwani licha ya athari mbaya ya vita nchini Ukraine, kufikia Septemba 2022, tathmini za maisha zilibaki juu zaidi baada ya Urusi kuinyakua Crimea mwaka 2014, na ripoti inasema kusudi la pamoja la ukarimu, na imani kwa Ukraine linaungwa mkono na Viongozi wengi wa Kimataifa.

Taarifa hii imeandaliwa kwa mdsaada wa vyombo mbalimbali vya Habari.

CA yalaani vituo vya Luninga kufutiwa leseni
Nasreddine Nabi: Hatujamaliza kazi Afrika