Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako amesema kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni hapo serikali ilifanyaUchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao.
”uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II – 248), na ndio watakao rudi chuoni hapo”, -Ndalichako.
Aidha amesema wanafunzi 4,586 wa mwaka wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya Ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na masomo yao.

Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.

Wanafunzi 290 waliokuwa wanasoma Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana sifa stahiki wametakiwa a kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo nazo kwenye vyuo vingine watakavyo.

Aidha Serikali imesema itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaorejeshwa UDOM na wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali watapewa mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya Ualimu itakayolipwa moja kwa moja Chuoni.

Serikali  ilifikia hatua ya kuwarejesha nyumbani wanafunzi 7805 mwezi wa tano waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati Chuo Kikuu Dodoma, huku sababu mbali mbali zikitajwa kuwa mgomo wa walimu huku pia ikisemekana ni wanafunzi hao kutokua na vigezo vya kusoma chuoni hapo mei 28.
Jipu lingine laiva: Wanafunzi Marehemu, waliofukuzwa chuo waombewa fedha za field
Watu Wanajaribu Kutengeneza Bifu Kati yangu na Diamond- Chameleone