Serikali, imeitaka Bodi mpya ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), kuimarisha usimamizi wa mitihani na mifumo ya utoaji taarifa ili kuondoa changamoto zinazojitokeza katika mitihani.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 11, 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda wakati akizindua Bodi hiyo na kusema pia inatakiwa kusimamia upokeaji taarifa za kulisaidia Baraza kupata changamoto mbalimbali ikiwemo za udanganyifu wa mitihani.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiongea wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo.

Amesema, “Endeleeni kuboresha mifumo ukiwemo ule wa usahihishaji kielektoniki, tunajua bado kuna changamoto tunapopeleka mitihani hivyo Bodi na Baraza endeleeni kufuatilia na kuhakikisha mnasimamia kwa kushirikiana na Kamati husika.”

Mwenyekiti wa Bodi ya NECTA, Prof. William Anangisye alisema watafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wa Elimu kwa uadilifu na ufanisi, ili kufikia malengo mapana ya Baraza la Mitihani na Serikali kwa ujumla.

Usikivu wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akiongea.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma, Upendo Rweyemamu naye ameahidi kuendelea kufanya kazi na Bodi mpya na ambayo imeundwa na Wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, na itahudumu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Julai 2022.

Afya ya uzazi ni changamoto kwa Mataifa
Shambilizi la bomu Ukraine lauwa watu sita