Nyota wa soka kutoka nchini  Zambia Rainford Kalaba ni kama kwa sasa hana mpango kabisa wa kusukuma kandanda barani Ulaya kama ilivyo kwa Mtanzania Mbwana Samatta anayetamba na KRC Genk ya Ubelgiji hii ni baada ya jana Jumatatu Kalaba kuongeza kandarasi mpya ya miaka miwili ya kuendelea kubakia TP Mazembe ya Congo DR.
Kalaba ambaye kwa sasa ndiye staa mkubwa kabisa katika kikosi cha TP Mazembe na mfungaji bora wa michuano ya shirikisho Afrika ameamua kubakia Lubumbashi mpaka Desemba 31, 2018 licha ya kupata ofa kadhaa za kucheza soka Ulaya.
Kalaba alijiunga na TP Mazembe mwaka 2010.Mpaka sasa ametwaa jumla ya mataji 12 yakiwemo mataji matatu ya DR Congo Super Cups,mataji matano ya ligi.Taji moja la klabu bingwa Afrika,taji moja la kombe la shirikisho Afrika na mataji mawili ya CAF Super Cups.
Aidha Kalaba ni mmoja kati ya wachezaji watatu walioingia kwenye fainali ya kumsaka mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ambapo mshindi atatangazwa Januari 5 huko Abuja, Nigeria.
Utumbuaji majipu wageukia mahakimu
Ligi Kuu Soka Ya Wanawake Tanzania Bara Kuendelea